Chapuo la Insha
Chapuo la Insha ni kitabu kinachochanganua kwa kina na mapana mbinu bora za uandishi wa insha kwa wanafunzi wa shule ya msingi. Kimeangazia changamoto mbalimbali zinazowakumba wanafunzi katika uandishi wa insha na kutoa suluhisho la kukabiliana na kila changamoto. Chapuo la Insha ni kitabu ambacho kimewasilisha mifano mbalimbali ya insha zenye mvuto wa kipekee unaochangiwa na ustadi wa hali ya juu wa kuyasuka matukio ya visa katika mazingira mbalimbali. Kitakuza na kuboresha msamiati, sarufi, ubunifu, umilisi wa mawasiliano katika lugha ya Kiswahili na maadili mbalimbali. Visa vya kitabu hiki vinaibua mijadala ambayo itakuza stadi ya kusikiliza, kuzungumza, kusoma na kuandika huku vikimwacha mwanafunzi na hamu na ghamu ya kujifunza zaidi. Kitabu hiki pia kitawafaa walimu katika kuwaelekeza wanafunzi kuwa waandishi mahiri.
KES 200
International delivery
Free click & collect
UPC | 9789966140081 |
---|---|
Author | Hellen Kangai |
Pages | 136 |
Language | Swahili |
License period | 1095 |
Format | |
Publisher | Queenex Publishers Ltd |
SKU | 9789966140081 |
None